UCHAGUZI – MKUTANO MKUU JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHAMPTON TAREHE 19 AGOSTI 2017

UCHAGUZI – MKUTANO MKUU JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHAMPTON TAREHE 19 AGOSTI 2017

HABARI MPASUKO ZA MWEZI AGOSTI 2017 TOKA UK.

Ndugu wana Northampton kwa mujibu wa taratibu na kanuni tulizojiwekea na matarajio yetu ya muda mrefu, Kwa niaba ya kamati ndogo ya maandalizi naitisha Mkutano Mkuu na wa Uchaguzi wa Viongozi Wapya wa Jumuiya yetu ya Watanzania Wote waishio Northampton na maeneo ya Wellingborough, Kattering na Corby [NORTHAMPTONSHIRE]
utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/08/2017

UKUMBI

Mkutano utafanyika katika ukumbi wa Norfolk Terrace, Semilong, Northampton NN2 6HS

MUDA

Kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) mpaka saa mbili usiku (8.00pm)

Kutakuwa na Chakula na Vinywaji Wakati Wote

Kamati ya maandalizi inaomba ushirikiano wenu ili Kuepuka kupoteza muda siku ya mkutano, Tunaomba kila mjumbe mwenye ajenda ya ziada yeyote ambayo angependa iwepo katika kikao chetu basi asisite kunipatia siku nne kabla ya mkutano kwa njia ya Barua Pepe kwenda;

suleimansalum160@yahoo.com au kwa kupiga simu ya Mkononi nambari 07963549935

 

MGENI RASMI

Ndugu ABRAHAM SANGIWA

Mwenyekiti – Tanzania Diaspora Community/Association in the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland

Atatoa ufafanuzi wa jinsi Jumuiya zetu hapa Northampton zitakavoshirikiana na Jumuiya hii kuu katika malengo muhimu yanayotugusa wote Kama Watanzania tunaoishi Ughaibuni ili kupata ufumbuzi wenye nguvu zaidi kwa ushirikiano wetu.

Tujitahidi kuzingatia muda siku hiyo.

“Umoja ni Nguvu”

Suleiman Salum

Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton[/vc_column_text][/vc_column][/vc_row]


X