RAMADHANI KAREEM 2019 TOKA TZUK – UINGEREZA.

RAMADHANI KAREEM 2019 TOKA TZUK – UINGEREZA.

Ndugu Wanafamilia na Watanzania Waishio UK

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza – TZUK DIASPORA Ndugu Abraham SANGIWA, pamoja na Uongozi mzima wa TZUK wanawatakia waislam wote duniani mwezi mtukufu mwema wa Ramadan- 2019.

Uvumilivu na huruma ambavyo ni maadili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote ule.”

Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti Ndugu Sangiwa amesema, “naomba tutumie mwezi huu wa kujitafakari kwa kukumbuka watu waliopoteza maisha wakati wakisaka usalama na hifadhi na tuonyeshe uungwaji mkono kwa mamilioni ambao wamefurushwa makwao au kupoteza maisha kwa sababu ya vita, ugaidi au mateso na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na familia zao hasa watoto wadogo wasio na hatia .”

Pia Mwenyekiti Ndugu Sangiwa amewasihi na kuwaomba Watanzania tunaoishi hapa UK na maeneo mengine ulimwenguni kuonyesha mshikamano na upendo kati yetu na kwamba mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unatuma ujumbe muhimu zaidi hii leo ya kwamba, “kile kinachotuunganisha kiimarike kuliko kile kinachotugawa.” ” Diaspora ya Watanzania Ughaibuni iwe chachu na mfano wa kuigwa nyumbani Tanzania. Mafanikio yetu kama Diaspora yatatokana na ukarimu, upendo pamoja mshikamano wetu na kuonyesha utofauti wa kuwa Wazalendo wenye fikra chanya kwa maendeleo ya Taifa letu.

TZUK tupo pamoja kwa Upendo na Amani

Abraham SANGIWA
………………………………….
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania UNITED KINGDOM

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


X