Mkutano Mkuu wa Watanzania Leeds Yorkshire na Humberside (TAYO) – TZUK DIASPORA

Mkutano Mkuu wa Watanzania Leeds Yorkshire na Humberside (TAYO) – TZUK DIASPORA

Kuendelezwa kwa Jumuiya ya Watanzania Leeds kwa Kuanzishwa rasmi kwa Jumuiya ya Watanzania waishio Yorkshire na Humber, na ushiriki wake

kwa Jumuiya kuu ya Watanzania UK {England, Wales, Scotland } na Northern Ireland.

Kufanya uchaguzi kuwachagua viongozi wa Kamati ya Jumuiya

Mkutano ulifunguliwa saa 10 jioni kwa wimbo wa ufunguzi na mjumbe Robert John London a kufuata kwa Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa muda wa Kamati ya maandalizi ya mkutano.

Hotuba ya Mgeni Rasmi ilifafanua:
Umuhimu wa kuanzishwa na kuimarishwa kwa Jumuiya za matawi (Local Communities) ili kuweza kuleta Umoja na Mshikamano miongoni mwa Watanzania,

kupitia Jumuiya kuu – TZUK DIASPORA ASSOCIATION/COMMUNITY
Sera ya Diaspora na kazi na juhudi zinazoendelea kufanyika kitaifa na kimataifa kwa kushirikiana vivile na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Maelezo ya kina kuhusiana na Katiba yetu ya Jumuiya ya Watanzania waishio UK na Northern Ireland (Tanzania Diaspora Community UK & NI – TZUK) yakifafanua ushiriki wa Jumuiya

za mikoani kwenye Baraza la Jumuiya kuu

Uchaguzi wa Viongozi

Vivile kulikuwa na maelezo ya kirefu kutoka kwa mwakilishi wa Leeds Swahili Culture Community Ndugu Saleh Salim kuhusu jumuiya yao na utayari wao wa kuwa pamoja katika Baraza la

jumuiya kuu ya Watanzania UK {England, Wales, Scotland } na Northern Ireland kuleta wawakilishi wao katika Baraza.
Majina ya wagombea yaliteuliwa na kupigiwa kura na Viongozi waliochaguliwa  ni hawa wafuatao:
Peter TIMAKELA
Mwenyekiti
Grace MUSINGA
Makamu Mwenyekiti
Dr Herbert HIZA
Katibu
Gertrude GOGADI
Mweka Hazina
Robert John LONDO
Mjumbe
Wawakilishi kwenye Baraza (The Council) Tanzania DiasporaAssociation/ Community UK & NI
Kwa mujibu ya Katiba ya Jumuiya kuu ya Watanzania UK {England, Wales, Scotland } na Northern Ireland , kila jumuiya za matawi/counties/town/cities UK na NI zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2)

watakaoingia moja kwa moja  katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK & NI

Wawakilishi wetu waliochaguliwa kwa kupigiwa kura ni hawa wafuatao:
Liliade MUNUO
Rashid LEMU

Maelezo mafupi na;

Dr Herbert HIZA
Katibu
Jumuiya ya Watanzania Yorkshire na Humber

X