JUMUIYA YA WATANZANIA LONDON (TA) YAPATA UONGOZI MPYA.

JUMUIYA YA WATANZANIA LONDON (TA) YAPATA UONGOZI MPYA.

HABARI MPASUKO ZA WIKI HII TOKA UINGEREZA
Jumuiya ya Watanzania wa London – TA {Tanzania Association – London} imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia siku ya *Jumamosi ya tarehe 15 July 2017 katika jiji la London.*
 *Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK {Great Britain & Northern Ireland}*
*Ndg Abraham Sangiwa.*
Viongozi waliochaguliwa ni hawa wafuatao:-
1. Dada Lynne Kimaro
Mwenyekiti
2. Ndugu Omwami George  Ndibalema
Makamu Mwenyekiti
3. Ndugu Lazaro Matiku
Katibu
4. Dada Halima Yusuph
Naibu katibu
5. Dada Edith Kimaro

Mweka Hazina

 

Picha Juu: Mwenyekiti wa TZUK Ndug. Abraham Sangiwa Akimpongeza Dada  Lynne Kimaro kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya TA – London

Pia kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & NI, kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae.

Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK

Asanteni,

*Uongozi*

*Tanzania Diaspora Community/Association – United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland*

X