JUMUIYA YA WATANZANIA READING- BERKSHIRE YAPATA VIONGOZI WAPYA.

JUMUIYA YA WATANZANIA READING- BERKSHIRE YAPATA VIONGOZI WAPYA.

HABARI MPASUKO ZA WIKI HII TOKA UINGEREZA

Jumuiya ya Watanzania wa Reading {Tanzania Reading – Berkshire Association- } imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia Kwa mujibu wa Katiba yake halali siku ya *Jumamosi ya tarehe 29 July 2017 katika jiji la Reading.*

Zoezi la Uchaguzi lilisimamiwa kikamilifu Kwa mujibu wa Katiba halali ya Jumuiya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi 2017 Ndugu Bernard Chisumo pamoja na timu yake chini ya Makamu Mwenyekiti na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Hussein Chang’a.

Katika hotuba yake fupi Ndugu Chang’a alisisitiza umuhimu wa wajumbe kuheshimu muongozo wa Jumuiya na kufanya shughuli zote za kwa kufuata muongozo waliojiwekea na kutokukubali kuyumbishwa na watu wachache wenye malengo binafsi.

 

*Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK {Great Britain & Northern Ireland}*

Ndugu Abraham Sangiwa

Ambae alisindikizwa na Makamu Mwenyekiti TZUK

Bi. Mariam Seif

Katika wasaa wake kwa Watanzania wa Reading Ndugu Sangiwa alisisitiza kuwa na umoja na mshikamano kwa Watanzania wote wanaoishi Reading- Berkshire na kuelezea kwa ufasaha jinsi TZUK inavyofanya shughuli zake kwa kushirikiana na jumuiya zote za mikoa hapa UK

Ndugu Sangiwa alielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kwa kushirikiana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania wanaoishi nje katika nchi mbalimbali duniani kupendekeza sera ya diaspora kwa pamoja itakayotoa majibu katika masuala mbalimbali yanayowagusa Watanzania Ughaibuni na mchango wao mkubwa kwa nchi yao mama “TANZANIA”, unavoweza kuwa katika mfumo utakaoleta manufaa makubwa kwa nchi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na huduma kwa jamii.

Tunahitaji kulinda na kutangaza utamaduni wetu na vivutio vya utalii kwa kuhakikisha vizazi vyetu ughaibuni vinanapata misingi muhimu na mafunzo kuhusu Tanzania ??

Ni muhimu sana kujenga “Model” itakayofanya TAIFA letu kufaidika na vizazi hivi vitakavokuwa na ” Exposure ” ya kimataifa katika nyanja mbalimbali zenye manufaa makubwa kwa nchi yetu, alisisitiza Ndugu SANGIWA.

*VIONGOZI WAPYA WALIOCHAGULIWA KUONGOZA JUMUIYA YA WATANZANIA READING – BERKSHIRE*

*MWENYEKITI*

NDUGU JOE J.E WARIOBA

*MAKAMU M/MKITI*

Bi. LAURA NOEL

*KATIBU MKUU*
Bi. Raya Walker

*NAIBU KATIBU* {KAIMU}

Peter Owino

*MTUNZA HAZINA*

Bi. FLORA DICKSON

*MTUNZA HAZINA MSAIDIZI*

Ndugu Elijah Mwamnyange

*WAJUMBE*

1: Peter Owino
2:MOHAMMED Upete
3: Paul Onyango
4: Geofrey Mumu
5: Evelyne Furzei
6: Dorine White.

*AUDITOR*

Eliud Mwijarubi

Pia kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & NI, kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae.

Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK

Asanteni,

*Uongozi*

*TA READING – BERKSHIRE*

Kwa  kushirikiana na

*Tanzania Diaspora Community/Association – United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland*

X